SIMBA, AZAM FC SASA SEPTEMBA 8, TIMU YAENDELE KUJICHIMBIA A-TOWN


KUTOKANA na shirikisho la soka Tanzania (TFF)  kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara, Simba itaendelea kujichimbia Arusha hadi Septemba 6 itakaporejea jijini Dar es Salam kwa ajili ya mechi yake ya kuwania ngao ya jamii dhidi ya Azam Fc itakayopigwa Septemba 8.
Awali Simba na Azam zilikuwa zicheze mechi hiyo Agosti 25 na kutokana na mabadiliko hayo wameliagiza benchi la ufundi la klabu hiyo kukutana ili kupanga program.