RUSHA ROHO BLOGU NDIO PA KUPERUZI

Asalam alaikum wadau.
Napenda kuwajulisha kwamba nimeanzisha blogu maalumu kwa ajili ya muziki wa taarabu.
Blogu hii inajulikana kwa jina la Rusha Roho na itakuwa ikielekezea mambo mbali mbali kuhusu muziki wa taarabu, ikiwa ni pamoja na historia ya wasanii wa muziki huo, habari 
zinazohusu maonyesho ya vikundi mbali mbali vya muziki huo pamoja na uchambuzi kuhusu mwenendo wa taarabu. Blogu hii inapatikana kwa anwani ifuatayo:
www.ramozaone.blogspot.com 
Nawakaribisha wadau wa muziki huo kutembelea blogu hii na kuchangia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutoa michango ya mawazo.
Natanguliza shukurani.
Rashid Zahor (Ramoza), 
Mmiliki wa blogu ya liwazozito.