RAGE AKUBALI KUITUMIKIA TFF


MWENYEKITI  wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amefuta uamuzi  wake wa kujiuzulu nafasi ya ujumbe katika kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
 Rage alitangaza kujuzulu nafasi hiyo hivi karibuni kwa madai kwamba kamati hiyo imeshindwa kusimamia sheria na kanuni za uendeshaji wa soka zinavyoeleza,kabla ya kuwasilisha barua yake kwa Rais wa TFF, Leodger Tenga.
 Rage amefuata uamuzi wake baada ya kukutana na Tenga na kuzungumzia mustakabali mzima wa jambo hilo na kumtaka aendelee kuwepo.