NUNUA SIMU ZA G-TIDE UPATE HUDUMA YA WAJANJA YA EASY TALK

 Meneja masoko wa kampuni ya G-Tide inayozalisha  simu za mkononi aina ya G-Tide  Mbwana Mtopa kushoto , pamoja na ofisa wa kampuni hiyo Chile Kasoga na Meneja wa G-Tide Nemes Kilegulo wakionesha wanahabari simu mpya ambazo unaweza kuunganishwa na huduma ya Easy Talk.KAMPUNI  inayozalisha simu za mkononi aina ya G-Tide  imehamasisha wananchi kununua simu zinazozalishwa na kampuni hiyo ili kujiunga na huduma mpya ya mawasiliano ya ujumbe wa sauti  ijulikanayo kama Easy Talk.
 Meneja Masoko wa kampuni hiyo Mbwana Mtopa alisema kwamba huduma hiyo ni nzuri na ya gharama nafuu ambayo inawawezesha watumiaji kuwasiliana pamoja kwa njia mbalimbali. 
Alisema kupitia huduma hiyo mteja wa mtandao wowote wa simu za mkononi nchini ambaye anatumia simu za G-Tide akijiunga na mtandao wa Intanet anaweza kuwasiliana na watumiaji wengine wa simu hizo kwa gharama za chini zaidi. 
Mtopa alisema mbali na ujumbe wa sauti, Easy Talk pia inahusisha kupunguza gharama ya kupiga simu kwa kuchat na watu pamoja na makundi tofauti. 
“Mfano umenunua intaneti katika mtandao fulani wa simu kwa MB 40 tu unaweza kutumia huduma zote za  Easy Talk kwa mwezi mzima,”alisema