NGOMA AFRICA BAND ILIVYOTINGISHA KATIKA TAMAHA LA ALAFIA HUMBURG, UJERUMANI


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU watatingisha jukwaa la ALAFIA Festival,mjini Hamburg,Ujerumani siku ya jumapili 26.8.2012 ,onyesho hilo kubwa la wazi linafanyika katikati ya kitovu cha mji wa Hamburg, eneo la Hamburg-Altona, ambapo patakua na pata shika ya nguo kuchanika.
Ngoma Africa band inashikilia award ya kimataifa " IDA-International Diaspora Award" kwa kuchaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika inayowakilisha vizuri kimataifa na kuwanasa mamilioni ya washabiki kila kona duniani,imetajwa mara nyingi kuwa bendi bora katika  maonyesho mengi ya kimataifa.
Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras makunja wa FFU,kwa sasa kinatamba na CD mpaya "Bongo Tambarare" ambayo inasikika katika kambi yao at www.ngoma-africa.com