MWANAMUZIKI ASHIMBA AIPUA ALBAMU YAKE MPYA 'WAKUKAYA' NCHINI FINLAND


Watayarishaji wa muziki wa Finland Bw Jussi Jaakonaho na Samuli Majamaki, wamefanya kazi na mwanamuziki  Ashimba's na kutoa albam mpya inayokwenda kwa jina la , "Wakukaya", kazi hii imefanyika kwa muda wa miaka mitatu na sasa iko tayari kabisa  kwa watu wa Ulaya, Tanzania na Afrika Mashariki na duniani kote  kwa ujumla wake,  albam hiyo imerekodiwa na kampuni ya muziki ya  Grandpop Records ya Finland.
(Picha na Tommi E. Virtanen)
Ashimba akikamua jukwaani wakati alipozindua albam yake nchini Finland katika jiji la Helnsinki  hivi karibuni.
Mwanamuziki Ashimba akiwa na baadhi ya wanamuziki aliofanya nao kazi jijini Helsinki.

Comments