MUSSA MGOSI ARUDI NYUMBANI

MSHAMBULIAJI wa Tanzania aliyekuwa anakipiga katika klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, Mussa Hassan Mgosi, anatarajiwa kuichezea timu ya JKT Ruvu katika msimu ujao wa ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba Mosi.
Mgosi aliyekwenda huko kucheza soka la Ridhaa akitokea klabu ya Simba amesajiliwa kwa maafande hao ambao aliwahi kuichezea zamani kwa mkataba wa miaka miwili.