MSIMU WA PILI WA TIKISA DANCE COMPETITIONPRESS RELEASE

TIKISA DANCE COMPETITION SEASON TWO 2012

POWER House Productions kwa kushirikiana na ITV, inatarajia kuendelea na utamaduni wake wa kuinua vipaji vya watu wanaopenda kudansi kupitia shindano la  TIKISA DANCE COMPETITION ambalo mwaka huu linafanyika kwa mara ya pili 2012.  
TISIKISA DANCE COMPETITION SEASON TWO – 2012, inawalenga  wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea. 
Usajili wa TIKISA DANCE COMPETITION SEASON TWO - 2012, utafanyika Agosti 31-Septemba 01 mwaka huu (Ijumaa na Jumamosi) ndani ya Hotel ya Kebby’s iliyoko maeneo ya Bamanga, Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi na kuendelea.  
Malengo ya TIKISA DANCE COMPETITION ni kuinua vipaji na kuwaendeleza washiriki waweze kubadili maisha yao kwa kutumia ujuzi wao wa kudansi. 
Kwa wote wanaotaka kuwa sehemu ya shindano hili wanakaribishwa.

Anne Iddrissu
Mkurugenzi Mtendaji
28 Agosti 2012