MAVETERAN WA SIMBA, YANGA TABATA KUKWAANA KESHO KATIKA MAADHIMISHO YA SIMBA DAY

MAVETERANI wa klabu za Simba na Yanga waishio eneo la Tabata kesho watakwaana katika mechi maalum ya kuadhimisha Simba Day ambayo itafanyika katika uwanja wa Tabata Shule.
Mratibu wa mechi hiyo Rodgers Peter amesema leo kwamba mchezo huo utapigwa asubuhi kabla ya baadaye kwenda uwanja wa Taifa kuungana na mashabiki wengine wa Simba katika maadhimisho la Tamasha hilo.