MASHUJAA MUSICA KUVAMIA MBEYA, RUVUMA WIKIENDI HII

BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wana kibega wiki hii watakuwa na ziara maalum katika mikoa ya Mbeya na Ruvuma kwa ajili ya kutambulisha wanamuzi wao wapya.

Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin
Sospeter, alisema kuwa wanamuziki wa bendi wataondoka kesho Alhamis kuelekea Songea mjini Mkoani Ruvuma.

Sospeter alisema onesho la kwanza litafanyika kwenye Ukumbi wa Serengeti  Club  uliopo mjini Songea.

Alisema Jumamosi watakuwa kwenye ukumbi wa Live uliopo Mbeya Mjini na Jumapili watamalizia ziara yao kwa bonanza maalum litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mbeya City Pub uliopo Mbeya mjini.

Sospeter alisema kuwa katika ziara hiyo inalengo la kutambulisha  safu mpya ya bendi hiyo na mtindo wao mpya wa Kibega.

Alisema kuwa bendi hiyo itarejea Dar es Salaa Jumatano na 
kuendelea na ratiba zake nyingine.

Bendi hiyo hivi karibuni ilifanya mabadiliko makubwa kwa 
kuchukuwa wanamuziki wapya ambao ni Charles Gabriel 'Chalz Baba', Soud Mohamed MCD' na Lilian Tungaraza Lilian Internet wote kutoka The African Stars Twanga Pepeta.

Wengine ni Saulo John kutoka katika bendi ya Extra Bongo na Ali Akida ambaye alikuwa mwanamuziki huru.