MANJI AVUNJA KAMATI NDOGO ZA YANGA, KAPTEN MKUCHIKA AULA


Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amevunja kamati ndogo ndogo ambazo ziliundwa na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Manji alisema kuwa kamati nyingine zitaundwa mara baada ya kamati ya utendaji Yanga kukutana na kuteua wajumbe wapya wa kamati hizo.
Kama hiyo haitoshi, Manji ameteua wajumbe watatu wa kamati ya Utendaji wakiwemo Isack Chanji na Mohamed Nyenji huku mwingine atatajwa baadaye.
Aidha, katika bodi ya udhamini ambayo itakuwa ikisimami kila kitu cha klabu hiyo, wamewaongeza, Kapten George Huruma Mkuchika, Seif Mohammeg 'Magari' na Balozi Ammy Mpungwe.