MAFTAH AMBADILI KAPOMBE STARS

NYOTA wa Simba Amir Maftah ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kuchukua nafasi ya nyota mwenzake wa Simba, Shomary Kapombe.
Stars iliingia kambini juzi kujiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki  itakayopigwa ugenini Agosti 15.
Meneja wa Stars Leopard Taso Mukebezi amesema leo kwamba hatua hiyo inafuatia Kapombe kuchanika Nyama za paja.
Aliongeza kuwa wachezaji wengine wote walioitwa katika kikosi hicho wanaendelea vema, huku wachezaji kutoka TP Mazembe Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakishindwa kuripoti mpaka sasa.