JAHAZI MODERN TAARAB KUTAMBULISHA RAP MPYA J'2


MKURUGENZI Mkuu wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf ‘Mfalme’  amepanga kutambulisha vionjo na rapu zao mpya, kwenye tamasha lililopangwa kurindima Jumapili, Agosti 26, kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Yussuf alizitaja baadhi ya rapu hizo kuwa ni ‘Yamemnogea’ pamoja na ‘Upatanisho’, ambazo zitakuwamo kwenye vibao vya albamu yao ijayo watakayoifyatua baadae mwaka huu, itakayokuwa na vibao sita.