FFU NGOMA AFRIKA BAND YATWAA TUZO YA BAND BORA AFRIKA


Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani,Bendi hiyo maarufu barani ulaya itatingisha tena jukwaa la onyesho ya kimataifa la International African festival ,mjini Tubingen,Ujerumani.
siku ya jumamosi 11-08 na jumapili 12-08-2012 katika uwanja wa  FestPlatz, Tubingen.
Habari za uhakika zinaeleza kuwa bendi hiyo imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya na kushinda tuzo la Award ya "IDA - International Diaspora Award". tuzo hilo litakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri Kamanda Ras Makunja usiku wa Jumapili 2012,Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa
kura nyingi na washabiki,pamoja na tahasisi mbali mbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kutumia muziki wake kama daraja na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki na kuwaunganisha  washabiki wa mataifa mbali mbali duniani.
Pia kikosi kazi hiko kimetajwa  mara nyingi kuwa kimediliki kujitoa muanga kwa kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na mazingira ya kivita !
kwa ujasili huu Ngoma Africa band inavuna inachopanda.
Ngoma Africa band imetajwa kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni ya washabiki na kuchangia kwa kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa rangi zilizomo kwa baadhi ya wazungu barani ulaya.
Ngoma Africa band inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50 dunia nzima,na washabiki wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi hiyo at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com
miongoni mwa wapenzi hao ni wapo wanawake na wanaume 
watoto ,vijana na wazee wenye rika na mataifa mbali mbali,
bila kujali itikadi za dini na matabaka ya maisha yao,wote wapo chini ya kivuli cha mzuka wa muziki wa Ngoma Africa Band aka FFU inayoongozwa na kamanda Ras Makunja aliyepindia akili kazi yake !
Tusikose kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com