BONANZA LA NANE NANE LASOGEZWA MBELE


Bonanza la michezo la nane nane soccer  bonanza lililokuwa lifanyike siku ya tarehe 8 mwezi wa 8 katika viwanja vya Tanganyika perkasi vilivyopo kawe jijini Dar es Salaam limesogezwa mbelea kwa ajili ya kupisha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Bonanza hilo litakaloshirikisha timu mbalimbali za mpira wa miguu, mpira wa mikono ( valleyball ) na michezo mingine mingi sasa linatarajiwa kufanyika baada hiki kipindi cha mfungo mwezi wa ramadhani kuisha.

Salum Suleiman, ambaye ndio mratibu wa bonanza hilo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za waandaaji wa bonanza hilo, SULE'S INC & ENTERTAINMENT zilizopo kawe jijini Dar es Salaam.

Suleiman amesema wamefikia uamuzi wa kalisogeza mbele bonanza hilo kutokana na maoni mengi ya wadau wa soka ikiwa ni pamoja na baadhi ya timu zitakazoshiriki bonanzna hilo kuomba kusogezwa mbele. "maoni mengi ya wadau na hata baadhi ya timu shiriki yamekua yakisisitiza kuomba kusogeza mbele bonaza hilo kwa sababu kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhani"

Aidha suleiman aliongeza kuwa maandalizi ya bonanza hili yalikuwa yamekamilika kwa asilimia kubwa ila kamati yake imefikia uamuzi wa kulisogeza mbele kutokana na kuheshimu mawazo ya wadau na hata wachezaji wenyewe "napenda kuishukuru kamati ya maandalizi ya Nane nane Soccer Bonanza kwani imeweza kukamilisha sehemu kubwa ya maandalizi ya bonanza hili ila kutokana na kuheshimu mawazo na maoni ya wadau walio wengi tumeamua kulisogeza mbele bonanza letu mpaka hapo mwezi wa ramadhani utakapomalizika"