BANC ABC KUWAFUNGULIA VISA PREPAID KADI WACHEZAJI WA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI BancABC SUP8R.


  Ofisa Masoko wa BancABC, Evelyn Augustine(kulia) akiwaelekeza wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar namna ya kutumia kadi ya VISA wakati wa zoezi la kuwafungulia wachezaji wote wa timu hiyo  huduma hiyo iliyofanyika katika tawi la Upanga Dar es Salaam
  Golikipa wa wa Mtibwa, Shaban Kado akiweka dolegumba katika moja ya fumu za BancABC wakati wa zoezi la kuwafungulia wachezaji wote wa timu hiyo huduma ya VISA iliyofanyika katika tawi la Upanga Dar es Salaam.
  Ofisa mahusiano kwa wateja wa BancABC, Said Ibrahamu (kulia) akiwaelekeza wachezaji wa mtibwa faida za Visa Prepaid kadi wakati wa zoezi la kuwafungulia wachezaji wote wa timu hiyo huduma ya VISA iliyofanyika katika tawi la Upanga Dar es Salaam.
  Ofisa mahusiano kwa wateja wa BancABC, Said Ibrahamu (kulia) akimkabidhi mchezaji wa mtibwa,Said Mkopi Visa Prepaid Kadi ambayo anaionyesha mara baada ya zoezi la kuwafungulia wachezaji wote wa timu hiyo huduma ya VISA iliyofanyika katika tawi la Upanga Dar es Salaam
  Ofisa Masoko wa BancABC, Evelyn Augustine(katikati) akiwaelekeza wachezaji wa timu ya Mtibwa faida ya kuwa na Visa Prepaid kadi wakati wa zoezi la kuwafungulia wachezaji wote wa timu hiyo huduma ya VISA iliyofanyika katika tawi la Upanga Dar es Salaam.


  
BancABC imetoa ofa ya kuwafungulia wachezaji wote wa timu zinazoshiriki mashindano ya BancABC SUP8R na kuwawekea kianzio kidogo cha huduma za kadi hizo ndani yake.
Akizungumza wakati wa kuwafungulia huduma hiyo wachezaji wa timu ya Mtibwa Suger ya Morogoro Ofisa Masoko wa benki hiyo, Evelyn Augustine alisema wamefanya hivyo ili kuwaweka karibu wachezaji hao wafahamu ubora na faida za huduma zitolewazo na benki inayowazamini katika mashindano wanayoshiriki ya BancABC SUP8R
Augustine alisema hii pia n I chachu hamasa kwa timu zingine ambazo hazikufanikiwa kuingia katika mashindano hayo wajitahidi awamu nyingine ambayo ni mwaka kesho wajitahidi na waweze kuingia kayika mashindano ya BancABC SUP8R ambayo yanafaida nyingi ndani yake kama hizi zainazotolewa sasa na bali na hizo ni pale tu timu inapofanikiwa kuingia katika mashindano hayo tayari inazawadi ya ushiriki ambayo ni shilingi milioni tano.
Wachezaji walipatiwa huduma ya VISA kadi mpaka sasa ni timu ya Mtibwa Suger ambayo inajumla ya wachezaji 20 na timu zingine wataendelea kuwapa huduma hiyo.