YANGA KUWAANIKA WARITHI WA MWAPE, ASAMOH KESHO

KLABU ya soka ya Yanga kesho itawatambulisha nyota wake wawili wapya wataoafunga pazia la usajili wa nmyota wa nje kupitia mchezo wao wa kirafiki dhidi ya JKT Ruvu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu ameiambia blogu hii kwamba nyota hao ni wale watakaoziba nafasi ya Mzambia Davies Mwape na Mghana Kenneth Asamoah awaliotupiwa virago hivi karibuni.
Hata hivyo, Sendeu hakuwa tayari kuwataja nyota hao kwa madai kwamba itakuwa 'Suprise' kwa mashabiki watakaojitokeza uwanujani hapo na kuwaomba wafike kwa wingi ili kuwashuhudia.
Kama hiyo haitoshi, mchezo huo utaonyesha kiwango ilichopfikia timu hiyo tangu kujiunga kwa kocha wake mpya Mbelgiji Tom Saintef mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mpaka sasa Yanga ina wachezaji watatu wa kimataifa ambao ni pamoja na Mghana Yaw Berko, Mnyarwanda Haruna Niyonzima na Mganda Hamis Kiiza.