WATATU KUCHUANA UENYEKITI YANGA

                                                                                 Manji

Jambele
KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imesema mpaka sasa ni wagombea watatu tu ndio wamepitishwa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo kupitia uchaguzi mdogo utakaofanyika JUlai 15 kwenye ukumbi wa Diamond Jubille jijini Dar es Salaam.
Katibu wa kamati hiyo Francis Kaswahili amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa ni wagombea wawili tu ndio wanaochuana katika nafasi hiyo.
Kaswahili amesisitiza kuwa wanaowania uenyekiti ni pamoja na Yusuf manji, John Jambele na Edger Chibura.