WANNE WAENGULIWA UCHAGUZI YANGA SC


WAGOMBEA wanne wanaowania uongozi katika klabu Yanga wameondolwa katika kinyang’anyiro hicho.
Habari zilizopatikana jioni ya leo toka kamati ya uchaguzi wa Yanga zinaeleza kwambawagombea hao wameonekana kuwa na dosari zilizobainiwa na kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanznia (TFF).
Wagombea hao ni pamoja na Sarah Ramadhan anayewania nafasi ya Uenyekiti pamoja na Zuberi Katwila, Waziri Gao na Ramadhan Kampira wanaowania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika julai 15 katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini dare s Salaam ambapo wagombea wwenye sifa wanaendelea na kampeni.