TPBO KUTOENDESHA MAPAMBANO YA NDONDI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANA [TPBO] INAPENDA KUWAARUIFU NDG WAPENZI WA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA KWAMBA KUELEKEA UJIO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UNAOTARAJIWA KUANZA WAKATI WOWOTE KULINGANA NA KALENDA YA KIISLAMU AU KUANDAMA KWA MWEZI, ,TUTASIMAMISHA MAPAMBANO YOTE NGUMI NDANI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

HII HAINA MAANA KWAMBA OFISI TETU ILIYOKO WILAYANI TEMEKE MWEMBEYANGA ITAFUNGWA ,BALI ITAKUWA WAZI KWA AJILI YA URATIBU WA MAPAMBANO YOTE AMBAYO YATAFANYIKA BAADA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWISHA.


TPBO  INAWATAKIA WAISLAMU WOTE NCHINI TANZANI MFUNGO MWEMA WA RAMADHANI NA PIA MWENYEZI MUNGU AWAJAALIE AFYA NJEMA ILI WAFUNGE MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI BILA MATATIZO YOYOTE.

IMEANDIKWA NA KULETWA KWENU NAMI;-
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS -TPBO
+255-713-644974