TFF YAWAPONGEZA VIONGOZI WAPYA YANGA SC

 Yusuf Manji -Mwenyekiti mpya wa Yanga 
 Clement Sanga- Makamu Mwenyekiti
 Abdallah Bin Kleb- Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
 George Manya-Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
Aaron Mwinula Nyanda-Mjumbe wa Kamati ya UtendajiShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. 
Ushindi waliopata wajumbe wapya sita waliochaguliwa kuingia kwenye Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wanachama wa Yanga waliohudhuria uchaguzi huo walivyo na imani kwao. 
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambayo hivi sasa ina vinara wapya, na kwamba wana changamoto kubwa ya kuhakikisha wanaendesha shughuli za klabu hiyo kwa kuzingatia katiba na kanuni. 
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga chini ya Jaji Mkwawa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na kanuni.