TBL YAMWAGA MIL.20 KUFANIKISHA MKUTANO MKUU WA SIMBA SC


Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala ya Sheria wa Kampuni ya Bia (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange (kushoto) hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika tarehe 5 Agosti mwaka huu. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe na Katibu wa Simba, Evodius Mtawala.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
25/7/2012

Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake kwa klabu ya Simba, bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu hiyo kwa ajili ya mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 5,  mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi hundi hiyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Kilimanjaro Premium Lager inatambua wajibu wake na ina nia ya dhati kuendeleza soka nchini. Kwa kwa kuzingatia hilo tungependa kuona maendeleo ya Simba na ndio maana tunaiunga mkono klabu hii katika mkutano wake mkuu. Tunaamini kuwa mkutano huu utaimarisha uhusiano uliopo kati ya klabu na wanachama wake kwa kuwapa fursa ya kuhakiki mwelekeo wa klabu yao waipendayo.Kavishe alieleza zaidi, “Mtu anapoangalia historia ya klabu hii kongwe ambayo imejengeka kutokana na rekodi nzuri ya mafanikio kwa muda mrefu utaona kwamba ina mamilioni ya wapenzi nchini. Soka ndio ndio mchezo mkubwa zaidi hapa Tanzania na bia ya Kilimanjaro imekuwa ikitoa mchango mkubwa kusaidia mchezo huu na ndio maana leo tunasaidia mkutano mkuu wa Simba ili kusaidia kudumisha uwajibikaji wa klabu kwa wanachama wake.
“Tunatambua wajibu wetu kama wadhamini wakuu wa Yanga katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio”.
MWISHO

Comments