SIMBA YAPIGWA 2-0, AZAM SARE

URA ya Uganda imeichapa Simba SC mabao 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
URA ilipata mabao yake kupitia kwa Owen Kasuule dakika ya 11 Feni Ally dakika ya 90+2.
Katika mchezo huo, Simba ilicheza vizuri, lakini tu walishindwa kutumia vizuri nafasi walizopata na mabao yote walifungwa wakitoka wao kushambulia.
Kikwazo kwa Simba leo alikuwa ni beki Derrick Walullya ambaye msimu uliopita alichezea Simba, akatemwa kwa madai kiwango kimeshuka. Aliwatia mfukoni washambuliaji wote wa Simba. 
Katika Uwanja wa Chamazi, Azam FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mafunzo, bao lao lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’dakika ya 26.   Katika mchezo wa kwanza, Chamazi Vita Club imeifunga 7-0 Port ya Djibouti.
URA baada ya kupata bao la pili refa akiwazuia kushangilia muda mrefu warejee uwanjani kuendelea na mchezo


Mussa Mudde anatia krosi


Sunzu anapiga mishe