SIMBA YAJITETETEA KUTOLEWA KOMBE LA KAGAME


KOcha mkuu wa Simba Milovan Cirkovic na msemaji wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga

SIKU moja baada ya kutolewa katika michuano ya Kagame kwa klabu ya Simba, uongozi wa klabu hiyo umewataka mashabiki na wanachama kutulia kwani kikosi hicho ndio kinasukwa. 
Makamu Mwenyuekiti wa Simba imu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wengi wageni hivyo bado timu haijawa katika mfumo mmoja. 
Alisema hali hiyo ndiyo ilichangia kufanya vibaya kwa timu hiyo katika michuano ya Kagame ambapo Simba ilimalizia mbio zake katika hatua ya robo fainali juzi baada ya kutolewa na Azam Fc kwa mabao 3-1. 
“Naomba mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hichi ambacho naamini kuna mengi yatatokea na hasa kwa wale wasioitakia mema timu yetu…napenda ieleweke kwamba kocha yupo katika kupanga kikosi na katika siku zijazo timu itakuwa madhubuti,”alisema Kaburu.