SIMBA USO KWA USO NA AZAM FC KESHO


MABINGWA wa ligi kuu soka tAnzania Bara Simba kesho jioni watacheza na mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC katika mchezo wa kuwania kombe la urafiki utakaopigwa kwenye dimba la  Amaan mjini Zanzibar.
Simba ambayo ilianza michezo hiyo jana kwa kuifunga Mafunzo mabao 2-1 imepania kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri, huku Azam nayo ambayo ilianza michuano hiyo jana kwa sare ya bao 1-1 na vijana wa Zanzibar nayo itahitaji kushinda mchezo huo.