SIMBA NA AZAM, YANGA NA MAFUNZO ROBO FAINALI KAGAME

Sunzu kushoto na Kapombe kulia wakimpongeza Boban
Na Prince Akbar
SIMBA imetoka sare ya 1-1 na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),  katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Felix Sunzu alikosa penalti dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, kufuatia beki mmoja wa Vita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini shuti lake lilipanguliwa na kipa Mcameroon, Lukong Nelson kabla ya mabeki wake ‘kuosha’.
Hadi mapumziko, Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lilifungwa kwa penalti na Etikiama Taddy, dakika ya 35, baada ya Juma Said Nyosso kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Simba ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrick Kanu Mbivayanya dakika ya 66.
Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo dakika ya 27, baada ya mshambuliaji wake Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ kuumia kifundo cha mguu na kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Kiggi Makassy.
Kwa matokeo hayo, Simba imemaliza kama mshindi wa tatu katika Kundi A na iytamemnyana na Azama katika Robo Fainali, wakati mabingwa watetezi Yanga watamenyana na Mafunzo.
Robo Fainali nyingine zitakuwa kati ya URA na APR na Atletico dhidi ya Vita.
Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde/Salim Kinje, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Abdallah Juma na Kanu Mbivayanga/Haruna Moshi.
AS Vita; Lukong Nelson, Ilo ngo Ilifo, Issama Mpeko, Ebunga Simbi, Mutombo Kazadi, Lema Mabidi, Etekiama Taddy, Mapuya Lema, Magola Mapanda, Basilua Makola, Mfongang Alfred SOURCE: http/bongostaz.blogspot.com