SIMBA, EXPRESS SARE SARE MAUA

MABINGWA wa ligi Tanzania Bara, Simba SC na mabingwa wa Uganda Experess jana wameshindwa kuonesha nani mkali baada ya kulazimisa sare tasa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hiyo ni mechi ya pili kwa timu hizo kukutana ambapo awali ilikuwa wiki iliyopita kwenye dimba la Kambarage mjini Shinyanga na kutoka sare ya bao 1-1.
Kupitia mchezo huo Simba iliwatumia baadhi ya wachezaji wake wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao mpya wa ligi kuu batra na michuano ya kimataifa wakiwemo   kiungo Patrick Kanu Mbivayanga kutoka DRC, Mussa Mudde, Abdallah Juma na wengineo.
Simba imeondoka leo kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya Urafiki ambapo jioni ya leo itaakwaana na Mafunzo ya huko.