SIMBA, AZAM FC SASA KUKIPIGA UWANJA WA TAIFAMECHI ya fainali ya kombe la Urafiki baina ya Simba na Azam Fc sasa litapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imefahamika.
Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika siku ya Alhamis kiwenye uwanja wa Aman Visiwani Zanzibar lakini baada ya majadiliano ya uongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na uongozi wa Simba na Azam wamekubaliana kulihamishia jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema mchana huu kwamba kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo na kitahakikisha kinashinda mchezo huo na kutwaa yubingwa.
Kamwaga alisema, kupitia michuano hiyo, Kikosi cha Suimba kimeweza kuimarika ipasavyo kadiri siku zinavyosonga hivyo ni wazi kwamba ubingwa utabaki Msimbazi.
ALisema mchezo huo unatarajiwa kuanza kupigwa saa moja usiku.