SAINTEF AANZA KWA NEEMA YANGA SC, MASHABIKI WAPIGWA CHANGA LA MACHO

KOCHA mpya wa klabu ya Yanga Tom Sentief ameanza vema na klabu hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Timu hizo zilikuwa zikuikwaana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki ambapo mabao ya Yanga yalipachinkwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' na Hamis Kiiza.
Kutokana na matokeo hayo, Saintef amewapongeza wachezaji wake na kusema kasoro ndogo alizoziona atazifanyia marekebisho kabla ya kuanza kwa michuano ya Kagame ambapo timu yake inashiriki kama bingwa Mtetezi.
Aidha, Mbelgiji huyo pia amekimwagia sifa kikosi cha JKT Ruvu na kusema kwamba pamoja na kufungwa kilionyesha kandanda safi. 
Katika hatua nyingine, mashabiki wa Yanga wamepigwa na butwaa baada ya kutoonekana mkwa wachezaji wapya wa kimataifa kama ilivyotangazwa jana na msemaji wa Yanga Louis Sendeu.
Sendeu aliwaambia waandishi wa habari kwamba katika mchezo wa leo Yanga ingetambulisha rasmi nyota wake waili wa kimataifa ambao wangeziba pengo la Mghana Kenneth Asamoah na Mzambia Davies Mwape ambao walitupiwa virago.