RAIS KIKWETE AAHIDI KUSAIDIA ZAIDI SEKTA YA MICHEZO, ATEMBELEA KAMBI YA TAIFA YA OLIMPIKI LONDONRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuendelea kusaidia sekta ya michezo na kuleta makocha zaidi wa kigeni nchini ili kuinua michezo. Rais Kikwete, alisema hayo jana alipokutana na wachezaji sita wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya michezo mbalimbali waliopo London, Uingereza tayari kushiriki michezo hiyo inayotarajiwa kwanza Julai 26, mwaka huu. Rais Kikwete, aliyeambatana na mkewe, Mama Salma, amewapa moyo wachezaji hao na kuwatakia kila la heri, waipeperusha vyema bendera ya Tanzania. Rais JK yupo England kwa ziara ya kikazi. Pichani ni Rais Kikwete (katikati) akiwa na wachezaji wa timu hiyo ya taifa ya Olimpiki, jana mjini London.   
JK, mama Salma JK na Balozi wa Tanzania, England, Peter Kallaghe (wa sita kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na maafisa wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki, leo jijini London. 


Rais JK akizungumza leo jijini London na wachezaji na maafisa wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki.


JK akiteta leo jijini London na Balozi Kallaghe wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa itakayoshiriki Olimpiki.