POULSEN AWAONA KWA MACHO MATATU ABDALLAH JUMA, BAHANUZI

KOCHA wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Mdenmark Kim Poulsen ameonesha kuvutiwa na viwango vya baadhi ya wachezaji wa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kombe la Kagame wakiwemo washambuliaji wa Simba na Yanga, Abdallah Juma na Said Bahanuzi.
Kim alisema wachezaji hao wameonesha viwango vya hali ya juu katika timu zao hivyo huenda akawaita katika kikosi cha timu hiyo atakachokitaja hivi karibuni.