OKWI MALI YA SIMBA HADI 2013, YANGA WATAJIBEBA

 Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange 'Kaburu' akionyesha mkataba wa mshabuliaji wao wa Kimataifa Mganda Emmanuel Okwi ambaye amezushiwa kujiunga na mahasimu wao Yanga na kusema kuwa nyota huyo anamkataba na Simba hadi 2013.

Kaburu akiwasikilzisha waandishi wa habari mahojiano 'live' na Okwi kutoka Uganda hivyo kuondoa utata kwamba nyota huyo yupo bongo na amesajiliwa Yanga.