NYOSSO ALEKEA KIBLA MWENYEWE MSIMBAZI

HATIMAYE beki wa Simba Juma Nyoso amekubali kumwaga wino wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
Hatua hiyo inafuatia majadiliano ya muda mrefdu baina yake na uongozi wa Simba ambapo taarifa zinaeleza kwamba Nyoso alianza kuleta 'mapozi' baada ya kuona Kelvin Yondan ametimkia Yanga.
Mmoja ya viongozi wa Simba alisema kwamba pamoja na Nyoso kuwa katika hatihati ya kutemwa baada ya kocha mkuu wa Milovan Circkoviv kutomkubali, alijiona lulu baada ya nafasi hiyo kuwa pungufu kutokana na kutimka kwa Yondan, lakini mwisho wa siku akamwaga wino mwenyewe.