NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME KUPIGWA KESHO ZOTENusu fainali zote mbili za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili jioni.