NGORONGORO KIMEO, YAPIGWA TENA NA RWANDA

Na Princess Asia
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes leo imefungwa mabao 2-1 na Rwanda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao ulikuwa wa marudiano ndani ya siku tatu, baada ya juzi.
Katika mechi hiyo ya kujipima nguvu kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Kocha Jakob Michelsen kabla ya kucheza na Nigeria katika mechi za mchujo za michuano ya Afrika, mabao ya Nyigu Wadogo yalitiwa kimiani na Nshimiyimana Emran katika dakika za pili na 30, wakati bao la kufutia machozi la Rwanda lilifungwa na Atupele Green dakika ya 71.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo iliitoa Sudan itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 29 mwaka huu dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rwanda ambayo inaundwa na wachezaji wengi waliocheza fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 miaka mitatu iliyopita tayari, mechi ya kwanza juzi Uwanja wa Chamazi, iliifunga Ngorongoro 1-0.