MWANACHAMA MAARUFU WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA


Mwenyekiti wa Simba, Mheshimiwa Ismail Aden Rage, anasikitika kutangaza kifo cha mmoja wa wazee wa klabu, Mzee Salum Pazi, kilichotokea jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 
Mzee Pazi ni mmoja wa waanzilishi wa Simba tangu enzi ikiitwa Sunderland. Msiba wa marehemu uko nyumbani kwake Manzese jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa leo. 
Akimzungumzia marehemu, Rage alisema alimfahamu Pazi tangu wakati yeye (Rage) akiwa mchezaji kwenye miaka ya 1970 na alikuwa mtu muhimu sana kwenye klabu. 
Kutokana na msiba huo, Simba itatoa Sh laki tano (500,000) kama ubani kwa familia ya marehemu.