MILOVAN ASEPA, WACHEZAJI WAJENGA MIILI

WAKATI kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba, Milovan Cirkovic akienda kwao Serbia, wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na mazoezi ya kujenga mwili 'Gym'.
Milovan ametimkia kwao kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya timu yake kutolewa katika hatua ya robi fainali ya michuano ya Kagame juzi anatarajiwa kurejea wiki ijayo na kuendelea na kazi yake ya kukinoa kikosi hicho.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wachezaji wa Simba wanaendelea na programu ya 'Gym' kabla ya Jumatatu kuhamia uwanjani na kuanza rasmi maandalizi ya michuano mbalimbali ikiwemo SUP8R banc ABC, Ligi Kuu bara na tamasha la Simba Day litakalorindima Agosti 8 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jiji ni Dar es Salaam.