MENEJA WA KLABU YA SIMBA, NICO NYAGAWA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

NAHODHA wa zamani wa klabu ya Simba ambaye sasa ni meneja wa timu hiyo Nico Nyagawa amepata pigo baada ya kufiwa na baba yake mzazi Mzee Menard Nyagawa asubuhi ya jana huko Makambako, Iringa.
Nyagawa amesema kwamba baba yake aliugua ghafla na kukimbizwa hospitalini jana hiyo kabla ya kukutwa na umauti huo.
"Ndio hiyo dada yangu hapa nipo njiani naelekea Makambako....taratibu zote nitajua nikifika huko,"alisema Nyagawa jana alipozungumza nami.
Blogu hii inampa pole Nyagawa na familia yake katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.