KUZIONA AZAM,SIMBA TAIFA KESHO BUKU TANO TU


KIINGILIO Cha chini cha mchezo wa fainali ya kombe la Urafiki baina ya Simba na Azam Fc utakaopigwa kesho jioni kimepangwa kuwa shilingi 5,000 kwa mashabiki watakaokaa viti vya kijani na bluu.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema watkaoakiaa viti vya odange watalipa sh.10,000, VIP C sh.15,000, VIP B sh.20,000 na VIP A sh.30,000.
Alisema tiketi zitaanza kuuzwa kesho katika vituo tofauti.
Timu bingwa itanyakua mil.10 na mshindi wa pili ataondoka na milioni 5.