KAMPENI YANGA KUANZA KESHO


WAKATI kampeni za kuwania uongozi katika klabu ya soka ya Yanga zikitarajiwa kuanza kesho, wagombea waliotakiwa kuwasilisha vyeti vya elimu za Sekondari wametimiza hilo.
Uchaguzi wa viongozi hao unatarajiwa kufanyika Julai 15 katika ukumbi wa Diamond Jubillee jijini Dar es Salaam.
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili ameiambia blog hii kwamba baada ya michakato yote ya awali kukamilika ambapo wagombea Sarah Ramadhan, Abdallah Binkleb, Edger Fongo, Omari Ndula, Waziri Ahmed, Mohamed Mbaraka na Ramadhan Kampira kuwasilisha vyeti vyao.
Kwa mantiki hiyo wagombea watakaochuana katika nafasi ya ujumbe ni pamoja na Jumanne Mwamenywa,, Edger Fongo, Beda Tindwa, Ramadhan Said,Omary A. Ndula,Shaban Katwila ,Ramadhan Y. Kampira ,Lameck Nyambaya,Peter H. Haule,Justine S. Baruti,Abdalah A. Mbaraka,
Yono Kevela,Mosess K. Valentino,Aaron Nyanda ,George M. Manyama,Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo na Gaudiusus Ishengoma.
Aidha nafasi ya makamu mwenyekiti itawaniwa na Ayoub Nyenze,Yono Stanley Kevela  na Clement A. Sanga huku nafasi ya uenyekiti itawaniwa na Jonh Paul Jambele,Yusuf Manji ,Edgar W. Chibula na Sara Ramadhan.