KAGAME LITAKUWA KOMBE LETU LA TATU MWAKA HUU-SIMBA SC


BAADA ya kutwaa ubingwa jana wa kombe la Urafiki, klabu ya soka ya Simba imesema itahakikisha inatwaa na kombe la Kagame ili kufikisha kombe la tatu ndani ya miezi mitatu.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo kwamba kikosi chake kimejipanga vema kushiriki michuano hiyo itakayoanza kesho na kusema kuwa wamedhamiria kutwaa taji hilo. 
"Tutahakikisha tunatwaa ubingwa huo ili kunyakua kombe la tatu mfulululizo ndani ya miezi mitatu, "alisema.
Awali Simba ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara, kabla ya juzi kutwaa ubingwa wa Urafiki.