JUSTIN BARUTI-APANIA KUILETEA MAENDELEO YANGA KAMA ATACHAGULIWA
Akiwa ni mwanachama wa Yanga ameamua kujitosa kuwania nafasi ya ujumbe katika klabu hiyo kwa lengo la kurejesha umoja na mshikamano ndani ya klabu hiyo. 
Baruti anasema katika umoja ndipo kunakuwepo na maendeleo hivyo uiwapo atachaguliwa atahakikisha anaimarisha umoja. 
Mbali na hilo, Baruti anasema iwapo atachaguliwa kuiongoza Yanga, kwa kushirikiana na viongozi wenzake watahakikisha wanaanzisha vitega uchumi ili kuifanya Yanga ijitegemee yenyewe na si kusubiri msaada wa wafadhili. 

Baruti ambaye ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa kampuni ya CMA kama Meneja uendeshaji, amewataka wanachama wa Yanga wachague viongozi wenye lengo madhubuti la kuisaidia klabu.