JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA SIKU YA SABA SABAMabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond  pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa.
Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni  Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na  Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D'  watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali