FFU ! NGOMA AFRICA BAND WAMALIZA KAZI DORTMUND, UJERUMANI


Dortmund,Ujerumani,
Wadau na wapenzi wa muziki katika maonyesho ya Afri-Ruhr Festival,siku ya jumamosi 30.06.2012 walijikuta wakizolewa na mdundo wa dansi wa bendi maarufu barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU, Kikosi kazi hiko kilifanikiwa tena kujiwekea rekodi ya pekee kwa kujizolea washabiki wanao ukubali mdundo wa bendi hiyo,baadhi ya washabiki walishindwa kujiziwia ! kwa utamu wa muziki walihamua kuvamia jukwaa.
Bendi maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja wa FFU,imejaa wanamuziki wenye bidiiakiwemo Soloist Afande Chri-B, Kikosi kazi cha Ngoma Africa kimezidi kujiimarisha kwa sasa ina idadi ya wanamuziki 14 ,ambapo zamani  ilikua na wanamuziki 8,wanamuziki wengi chipukizi wamejiunga
na Ngoma Africa band kwa nguvu moja ya kutaka kuimarisha na kuitangaza miziki ya Bongo na Afrika mashariki pia,Ngoma Africa band inaonekena ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya yenye kuwa na washabiki na waufuasi
wengi wa mataifa,umri mbali mbali, bendi ambayo washabiki wanadai kuwa ni mali yao ! na Ras makunja na wanamuziki ni watumishi wa washabiki tu.
Bendi hiyo maarufu kwa sasa wanatamba na CD mpya ya "Bongo Tambarare" ambayo ina nyimbo za "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" unaweza kuzisikiliza at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com