FFU NGOMA AFRICA BAND NA TUZO


Habari za uhakika zinatonya kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" au maarufu kwa jina la "FFU"wazee wa virungu na makombora ya muziki,yenye makao yake nchini Ujerumani, Bendi imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki ya Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu la" IDA - International Diaspora Award"  award , hiyo inatolewa na tahasisi za kimataifa,itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo KamandaRas Makunja wa FFU mwanzoni mwa mwezi wa nane.
Inasemekana Sherehe za kukabidhiwa TUZO hiyo zitafanyika mjini Tubingen,  mkoa wa Baden w├╝rttemberg, kusini mwa ujerumani.
Tahasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanziamwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika inayolitangaza bara
la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia ushindi wa mamlioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hiyi inakubalika na  mamilioni  ya washabiki wa mataifa mbali mbali, 
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni50 duniani kote,hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa,kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya washabiki,ni bendi ambayo kipenzi cha mamilioni ya washabiki. katika kambi yao hiiwww.ngoma-africa.com inakadiliwa kuwa na mamilioni ya lank.
Tunawatakia kila yaliyo mema vichaa wetuwww.ngoma-africa.com