FFU KUPELEKA HEWANI BONGO TAMBARARE NA SUPU YA MAWE


Wakati tunapoelekea katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba,watanzania tunafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya muziki wa dansi  Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani.
CD hiyo yenye nyimbo tatu  "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari"Inasemekana imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio
duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa,hili watanzania wenye Bongo Tambarare yawe wapate raha ya muziki.
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii, kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na  wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo afande Chris-B.
Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com