CHEKECHEA WA YANGA WATIMULIWA ZANZIBAR

CHAMA cha soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimeitimua timu ya Yanga kwenye michuano ya kombe la Urafiki inayoendelea Visiwani humo.
Msemaji wa ZFA Munir Zakaria amesema kwamba wameamua kuitimua timu hiyo kutokana na kuleta hasara tu kwani haileti mvuto wowote lwa mashabiki.
"Sisi tulialika timu ya Yanga lakini tunashangazwa na uongozi kutuletea timu ya Vijana, sasa uwepo wa timu hiyo hausaidii lolote katika kuleta hamasa ya michuano hiyo zaidi ya hasara tu kwani mashabiki walitegemea kuiona timu halisi ya Yanga,"alisema.