CECAFA YAFAGILIA WATANZANIA KUSAPOTI KAGAME

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye (Kati)akizungumza na waandishi wa habari leo 


BARAZA la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limewapongeza Watanzania na vyombo vya habari nchini kwa kufanikisha michuano ya Kagame inayofikia tamati kesho kwa timu za Azam na Yanga kucheza fainali kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye amesema leo kwamba kujitokeza kwao uwabnjani na vyombo vya habari kuyaripoti vizuri kumechangia kuyafanya mashindano hayo kuwa bomba.
Aidha, Musonye amewapongeza wadau mbalimbali ikiwemo Serikali na hoteli mbalimbali kwa kuweza kuzihifadhi timu zilizoshiriki michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Julai 14 mwaka huu.