BURUNDI YAPATA MWAKILISHI WAKE MISS EAST AFRICA
Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Burundi katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu amepatikana. 
Mrembo huyo wa jijini Bujumbura anaitwa Miss Mugisha Nadege (21) ana urefu wa futi 5.71 ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha…..ambapo anasomea degree ya mawasiliano 
Mrembo huyo alitangazwa rasmi jana na mratibu wa mashindano ya Miss east Africa kwa Nchi ya Burundi ambae ni barozi wa amani Nchini Burundi Serge Nkurunziza ambaye alimtangaza baada ya mrembo huyo kuwashinda warembo wenzake waliojitokeza kutaka kushiriki mashindano hayo. 
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam