BEDA H.TINDWA:ANAYEUTAKA UONGOZI YANGA ILI KUONDOA UKATA



MGOMBEA huyu anasema  amejitosa kuwania nafasi hiyo ili kuweza kusaidia kutatua matatizo mengi yanayoikabili klabu ya Yanga ikiwemo mishahara ya wachezaji na kocha. 
Tindwa alisema hayo yatatimia iwapo wanachama wa Yanga watampa ridhaa ya kuongoza klabu hiyo. 
Kama nitachagulia nitasimama kidete kuhakikisha makocha na wachezaji wanalipwa mishahara kwa wakati kwani bila wao kulipwa ama kuhudumiwa vizuri hakuna mafanikio yoyote na ndio chanzo cha migogoro,”anasema . 
Kama hiyo haitoshi, Tindwa anasema iwapo atafanmikiwa kuongoza Yanga, atahakikisha anailetea klabu hiyo mafanikio ndani na nje ya nchi. 
“Mimi si ni mwanachama tu wa Yanga bali ni mwanamichezo mwenye uchu wa maendeleo, hivyo nitasimama kidete kuisaidia Yanga kujitegemea yenyewe,”anaongeza. 
Mbali na hilo, Tindwa amepania kusaidia kutafuta wachezaji mahiri watakaoitumikia klabu hiyo kama alivyofanya kwa Gula Joshua na wengine. 
“Napenda kuwasikhi wanachama wenzangu kwa kuchagua viongozi wenye kuisaidia timu yetu na si kutaka kujinufaisha,”alisema.

Comments